Saturday, May 16, 2009

Barabara ya Kuelekea East Zuu


Barabara ya kuelekea Iringa kupitia police line, central police, hazina x,kigamboni(kg estate) maghorofa mengi, mazengo(st.johns univeristy)kikuyu, chidachi almaruufu kama barabara ya kuelekea eeast zuu.....ni daladala/express/matatiu moja tu mpaka huku kutokea city centre

University of Dodoma

Kuanzishwa kwa chuo kikuu cha dodoma, kumeongezeka ukuuaji wa mji wa dodoma kutokana na kuwa na ongezeko la idadi ya watu mjni hapa,
chuo hichi kilichopo eneo la chimwaga km 7 kutoka dodoma mjni mpaka sasa kina wanafunzi wapatao elfu 9,000 na kinatazamiwa kuchukua hadi wanachuo elfu 45 pindi kitakapo kamilika.... kuongezeka kwa chuo hiki cha u Udom kunaufanya mji wa dodoma kuwa na vyuo vikuu viwiwli(University of Dodoma na St.John university), huku pia kukiwa na vyuo vingine viwiwli vya elimu ya juu ambavyo ni Chuo cha Elimu Biashara(CBE) na Chuo cha Mipango na Menedeleo vijijini(IRDP)......
idadi ya wakazi inazidi kuongezeka ktuokana na kupanauka kwa mji

Maktaba Kuu ya Dodoma

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya watu wanaotumia maktaba, serikali iliamua kujenga maktaba mpya na ya kisasa mjini dodoma itakayokidhi mahitaji ya watu waliopo mjini hapa..awali maktaba ilikuwa katika jengo la mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA, na kwa sasa imehamia katikas eneo lilokuwa stendi ya zamani ya mabasi katika eneo la makole hospital jirani na barabara ya kwanza na shule ya sekondari dodoma.... ukifika dodoma karibu maktaba mpya na ya kisasa

Nyerere Square


Nyerere Square ni eneo lililotengenezwa maalum kwa ajili ya kupumzikia na kupata viburudisho hasa unapokuwa katikati y amji huu..
eneo hili lipo katikati ya barabara ya 5 na barabara ya 6 almaarufu kama kuu street..
eneo hili zamani lilikuwa ndo soko kuu la mjini dodoma kabla ya serikali kulivunja na kuwahamishia katika eneo la majengo ambapo ndipo kulipojengwa soko kuu la kisasa mjin hapa.....
kwa mahitaji yako yote ya bidhaa na vyakula fika soko kuu la majengo amblo ni la kisasa kabisa na wafanyabiashara wapo katika mpangilio..

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipo hapa mjini Dodoma, jengo hili lipo katika eneo la makole kandokando mwa barabara ya morogoro, na jirani na Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE)..
ni mojawapo ya rasilimali na vivutio vya mji huu...
kipindi cha bunge shughuli nyingi hufanyika mjini hapa na kuwapatia wananchi riziki, huduma kama za vyakula sokoni, malazi, kumbi za burudani na biashara za nguo .....
karibuni Idodomya makao makuu matarajiwa ya serikali

Mmiliki wa eastzuu.blogspot.com

Baraka Kizuguto(Baf da Don!!)mmiliki wa blog yenu mpya ya eastzuu.blogspot.com
blog hii imeanzishwa kwa lengo la kuelezea na kuutangaza mji dodoma ambapo ndipo kunapopatikana eneo la east zuu.Nategemea sapoti yenu katika hili ili tuweze kulifanikisha hili
karibuni sana...kwa maoni, habari usisite kuniandikia bafmaks@gmail.com,or eastzuu@gmail.com,
pia unaweza kuzitembelea blog mama za www.kitaanikwetu.blogspot.com
kwa pamoja tukishikiriana naamini tunaweza!!!!!!!!!!!